Home
Tanzanian Stories
World News
Events
Classifieds
Photo Gallery
Downloads
Discussion Forum
Career Services
Links
Tanzania Safari
Powers Bongo Corner Porojo Page Politics
About Tanzania
National Park’s In Tanzania
Tanzania cities
Michuzi corner
Login Register
Shopping Cart
site designed and
developed by eIQ.net
Home > Powers Bongo Corner > Porojo Page

Kigoda na uroda

Friday, August 19, 2005 (UMST)

Uroda wa Dr. Kigoda
Watu husemaga kuwa siyo wote waitwao 'dokta' wameelimika. Nafikiri sasa naelewa kwa nini.

Watu husemaga kuwa siyo wote waitwao 'dokta' wameelimika. Nafikiri sasa naelewa kwa nini. Hivi itawezekana vipi 'dokta' Abdallah Kigoda atembee na mwanamke, asitumie tahadhari, ampatie mimba halafu aingie mitini, halafu akishtakiwa mahakamani eti na yeye atume polisi kumsumbua huyo mwanamke?

Mtu yeyote anayejua siasa huwa anatathmini matokeo ya matendo yake. 'dokta' bila shaka hajui jinsi ya kutathmini matokeo ya matendo yoyote. Angetoa 'kidogodogo' hapo awali haya mambo yasingefika mahakamani. Sawa, labda alijisahau na alikuwa 'bize' na shughuli za kiserikali au alikuwa 'bize' na kutia mimba wanawake wengine, lakini mtu mwenye kutathmini matokeo asingetuma jeshi la polisi kumsaka mwanamke huyo maana huko ndiyo ukisikia kuchochea moto.

Mchungaji Jesse Jackson alipogundulika kuwa alitembea na mwanamke na kuzaa nae mtoto alikimbia kutoa tamko. "I am truly sorry for my actions," he said. "I am father to a daughter who was born outside of my marriage." Tafsiri: 'Naomba msamaha kwa matendo yangu. Mimi ni baba wa mtoto wa kike niliyezaa nje ya ndoa yangu'.

Kwa nini Kigoda asiige mfano huu??? 'Dokta' Kigoda, unakumbuka jinsi Bill Clinton alivyojichimbia kaburi taratibu? Angefanya kama mzee jackson, yasingemkuta mambo ya kutishiwa kuachishwa kazi na wazee wa nchi yake.

Kigoda, najua wewe unajaribu kutunza heshima yako lakini nafikiri heshima yako ilipungua pale ulipoamua kuingia kitandani na mwanamke nje ya ndoa.

Kituko hiki kinatukumbusha kuwa nyie viongozi huwa hamvai mipira ya kiume wakati wa kufanya mapenzi. Mnatusihii tuache 'kula ndizi bila maganda yake'. Hivi sisi tutawatilia maanani kweli kama hamfanyi mnavyotuambia?

'Dokta' Kigoda naona sasa unaliona joto la jiwe na wewe sasa utakuwa mfano kwetu sote. Uliamua 'kula ndizi bila maganda yake' sasa unajuta. Kesho naomba uiingie bafuni na 'raincoat' yako. Ukishindwa na ukiona maisha machungu, jaribu 'kumumunya pipi na maganda yake'.

Nakutakia Idd El Fitri njema na mwaka mpya. Utanialika kwako kula mbuzi kwenye maulidi?? Au ndiyo utakwenda baa kwenda kuchunwa ngozi?


Add Your Comment

 
All content on this site is copywright by its respective owner.
All rights reserved. © 2005 mbongo.com  |  Terms of Use  |  Privacy Policy